Katibu Mkuu wa wizara ya
Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel
akifungua kongamano la vijana kutoka shule na vyuo mbalimbali nchini
lililobeba kauli mbiu ya “Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya
jamii” kuelekea maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa lililoandaliwa
na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika
ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Na Michael utouh
“Tuna kazi kubwa ya kujenga
fikra za vijana kwamba ili kufanikiwa katika maisha siyo
lazima
kuajiriwa, vijana wengi ukiwahoji wanakwambia changamoto kubwa
wanayoikabili ni ukosefu wa ajira. Lakini wanasahau kuwa changamoto zipo
nyingi zinazowakabili,” amesema.
Prof. Ole Gabriel amezitaja
changamoto nne zinazokabili vijana ambazo zinasababisha washindwe
kujiajiri au kushindwa kujiendeleza pindi wanapojiajiri kuwa ni, ukosefu
wa fikra kutokana kwamba wengi hawaziruhusu fikra zao kubuni mbinu za
kujiajiri. Changamoto nyingine aliyoitaja ni vijana kukosa uelewa, mbinu
na ubunifu wa kuongeza thamani ya shughuli wanazofanya.
Changamoto nyingine aliyoitaja
ni mfumo mbovu na usio rafiki kwa vijana hasa mifumo duni ya upatikanaji
mitaji na masoko, hususani katika kipindi hiki ambacho kuna wimbi kubwa
la vijana wasio na ajira.
Katibu Mkuu wa wizara ya
Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel
akisisitiza jambo kwa vijana walioshiriki kwenye kongamano hilo.
Ameshauri kuwa “Hivi sasa kuna
elimu ya ujasiriamali lakini niseme tu haitomsaidia kijana kujikwamua
sababu hutoa elimu ya uzalishaji pekee. Ili kijana afanikiwe na
ujasiriamali, kwanza inabidi apewe elimu ya kufanya utafiti wa bidhaa
inayohitajika kwa kipindi husika, akishajua bidhaa hitajika ndipo afanye
uzalishaji kisha hatua ya mwisho kutafuta masoko ambayo tayari
ameshayafanyia uchunguzi.”
Pia ameshauri vijana kuwekeza
katika biashara kilimo kwa kuwa ndiyo sekta pekee yenye fursa ya kutoa
ajira kwa wingi kwa kuwa imeajiri asilimia 84 ya vijana.
“Tanzania ina vijana zaidi ya
milioni 16.2 ni sawa na asilimia 70 ya watanzania, waliofanikiwa
kuajiriwa katika sekta binafsi ni milioni 1, waliojiajiri milioni 1.1
waliopo katika sekta ya umma ni 18,8000 na katika sekta ya kilimo wapo
vijana milioni 13.2 na bado nafasi zipo katika sekta hiyo,” amesema.
Mwakilishi kutoka Shirika la
Kazi Duniani (ILO), Annamarie Kiaga akizungumza machache kwenye
kongamano la vijana kutoka shule na vyuo mbalimbali nchini lililobeba
kauli mbiu ya “Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii”
lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es
Salaam katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Hata hivyo, Prof. Gabriel
amewaasa vijana kutotumia utandawazi vibaya hasa mitandao ya kijamii
kutokana kwamba imekuwa sababu ya vijana wengi kutokuwa na maadili.
“Utandawazi unabomoa uwezo wenu
wa kufikiri, zamani vijana walikuwa wanakimbilia kuwekeza katika sekta
ya kilimo ila sasa kutokana na utandawazi wanakimbilia kutafuta ajira
hata kama fursa hakuna,” amesema na kuongeza.
“Msipoangalia miaka michache
ijayo tutakuwa watu wa teknolojia na mitandao. Maadili mema
tuliyojengewa yatapotea kwa sababu ya kufikiri kwamba mitindo ya
kimaisha kutoka nje ndiyo inafaa kuliko ya kwetu, inabidi turudishe yale
maadili ya zamani sababu nchi yoyote isiyokuwa na maadili, tamaduni
imeparanganyika na haina maendeleo,” amesema.
Mwakilishi kutoka Shirika la
Kazi Duniani (ILO), Annamarie Kiaga akizungumza kwa niaba ya UN amesema
kuwa shirika hilo litahakikisha linawezesha vijana kushiriki katika
maendeleo ya uchumi kwa kuwainua kiuchumi pamoja na kutoa elimu ya namna
ya kujiajiri.
Mkurugenzi wa Idara ya
Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Celestine Mushy
akizungumza jambo kwenye kongamano la vijana kutoka shule na vyuo
mbalimbali nchini lililobeba kauli mbiu ya “Wajibu wa vijana katika
uchumi na maendeleo ya jamii” lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na
kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa
kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Mbunifu wa mavazi Johari Sadiq
akizungumzia jitihada, changamoto, fursa na mafanikio aliyoyapata katika
yake ajira binafsi kama mtoto wa kike, kwenye kongamano la vijana
kutoka shule na vyuo mbalimbali nchini lililobeba kauli mbiu ya “Wajibu
wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii” lililoandaliwa na Umoja
wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa
mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
MC maarufu nchini ambaye pia ni
Mhamasishaji Ujasiriamali, Anthony Luvanda akizungumzia ajira yake
binafsi na mafanikio aliyonayo kwenye kongamano la vijana kutoka shule
na vyuo mbalimbali nchini lililobeba kauli mbiu ya “Wajibu wa vijana
katika uchumi na maendeleo ya jamii” lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa
(UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa
kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Mwezeshaji ambaye ni
Mjasiriamali kijana Stella Imma, akizungumza kwenye kongamano la vijana
kutoka shule na vyuo mbalimbali nchini kuelekea maadhimisho ya wiki ya
Umoja wa Mataifa lililobeba kauli mbiu ya “Wajibu wa vijana katika
uchumi na maendeleo ya jamii” lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na
kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika kumbi wa mikutano wa
kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Mshauri na Mkufunzi wa
Ujasiriamali/Biashara wa Program ya anzisha na imarisha biashara yako
(SIYB) akitoa hamasa kwa vijana kutoka shule mbalimbali na vyuo
waliohudhuria kongamano la vijana kuelekea maadhimisho ya wiki ya Umoja
wa Mataifa lililobeba kauli mbiu ya “Wajibu wa vijana katika uchumi na
maendeleo ya jamii” lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika
jana jijini Dar es Salaam katika kumbi wa mikutano wa kimataifa wa
Julius Nyerere (JNICC).
Mwanafunzi Matilda Moses wa
kidato cha pili kutoka shule ya sekondari ya Gerezani akimuuliza swali
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante
Ole Gabriel (hayupo pichani) juu ya kusimamia maadili ya Kitanzania na
kuwaelimisha wazazi namna bora ya kusimamia malezi ya watoto wao jijini
Dar es salaam wakati wa kongamano la vijana kutoka shule na vyuo
mbalimbali nchini lililoandaliwa na Shirika Umoja wa Mataifa
linalishughulikia Maendeleo (UNDP).
Pichani juu na chini vijana
pamoja na wanafunzi kutoka shule mbalimbali wakiuliza maswali kwenye
kongamano la vijana kuelekea maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa
lililobeba kauli mbiu ya “Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya
jamii” lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini
Dar es Salaam katika kumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere
(JNICC).
Mkurugenzi wa Idara ya
Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (wa tatu
kulia) akifurahi jambo kwenye kongamano la vijana kuelekea wiki ya
maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa lililobeba kauli mbiu ya “Wajibu
wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii” lililoandaliwa na Umoja
wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika kumbi wa
mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Mwezeshaji MC Anthony Luvanda
akifurahi jambo kwenye kongamano la vijana kuelekea maadhimisho ya wiki
ya Umoja wa Mataifa lililobeba kauli mbiu ya “Wajibu wa vijana katika
uchumi na maendeleo ya jamii” lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na
kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika kumbi wa mikutano wa
kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Mkurugenzi wa Idara ya
Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Celestine Mushy
akiwatambulisha baadhi maafisa wa wizara hiyo waliochini ya idara yake
ambao ni vijana na wamepata nafasi ya ajira serikalini na kuwasifia
kwamba ni wachapakazi na hodari katika vitengo vyao wakati wa kongamano
la vijana kuelekea wiki ya maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa
lililobeba kauli mbiu ya “Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya
jamii” lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini
Dar es Salaam katika kumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere
(JNICC).
Vijana wakiwa wamejipanga huku
wakishikilia mabango ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwenye
kongamano la vijana kuelekea maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa
lililobeba kauli mbiu ya “Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya
jamii” lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini
Dar es Salaam katika kumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere
(JNICC).
Mkurugenzi wa Idara ya
Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akiwapiga
msasa vijana kuhusiana na Malengo ya Dunia kwenye kongamano la vijana
kuelekea maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa lililobeba kauli mbiu
ya “Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii” lililoandaliwa
na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika
kumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Picha ya pamoja.
Pichani juu na chini ni Sehemu
ya wanafunzi wa shule mbalimbali na vyuo vikuu walioshiriki kongamano la
vijana lililobeba kauli mbiu ya “Wajibu wa vijana katika uchumi na
maendeleo ya jamii” lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika
jana jijini Dar es Salaam katika kumbi wa mikutano wa kimataifa wa
Julius Nyerere (JNICC).
Baadhi ya maafisa wa Idara ya
Ushirikiano wa Kimataifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa katika picha ya pamoja wakati wa
kongamano la vijana kutoka shule na vyuo mbalimbali nchini lililobeba
kauli mbiu ya “Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii”
kuelekea maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa lililoandaliwa na Umoja
wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa
mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Post a Comment