Slaus Technologies Tz1
 

Harakati za jiji Harakati za jiji Author
Title: JESHI LA POLISI WILAYA YA TEMEKE, LEO LIMEWAKAMATA PANYA ROAD 14
Author: Harakati za jiji
Rating 5 of 5 Des:
Mwanafunzi wa Kidato cha Tatu wa Sekondari ya Lumo,Isack Ernest mwenye miaka 16 (katikati) akiwa na Kijana Menson Sombe wanaotu...



Mwanafunzi wa Kidato cha Tatu wa Sekondari ya Lumo,Isack Ernest mwenye miaka 16 (katikati) akiwa na Kijana Menson Sombe wanaotuhumiwa kuwa ni Panya Road wa kundi la Taifa Jipya  wakishuka kwenye kituo cha Polisi cha Chang’ombe wilayani Temeke jana baada ya kukamatwa juzi wakileta vurugu na kupora watu kwa kutumia mapanga kwenye tamasha la kuibua vipaji lililofanyika Uwanja wa Zakhiem Mbagala . (PICHA ZOTE NA ELISA SHUNDA)



Vijana wanaotuhumiwa kuwa ni Panya Road wakiongozwa na askari polisi kushuka kwenye gari walipofikishwa katika kituo cha Polisi cha Chang’ombe wilayani Temeke jijini Dar es Salaam jana.

 Vijana wanaotuhumiwa kuwa ni Panya Road

 Mwanafunzi wa Kidato cha Tatu wa Sekondari ya Lumo,Isack Ernest mwenye miaka 16 (kulia) anayetuhumiwa kujihusisha na kundia la Panya Road akitoa maelezo kwa waandishi wa habari jinsi alivyojikuta amezimia na kuzindukia mochwari baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira kali katika kituo cha Polisi cha Chang’ombe wilayani Temeke jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke,Kamishina Msaidizi (SACP),Gilles Murato.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke,Kamishina Msaidizi (SACP),Gilles Murato akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kukamatwa kwa vijana ambao wanatuhumiwa kuwa ni Panya Road wa kundi la Taifa Jipya katika kituo cha Polisi cha Chang’ombe wilayani Temeke jana baada ya kukamatwa juzi wakileta vurugu na kupora watu kwa kutumia mapanga kwenye tamasha la kuibua vipaji lililofanyika Uwanja wa Zakhiem Mbagala.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke,Kamishina Msaidizi (SACP),Gilles Murato akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kukamatwa kwa vijana ambao wanatuhumiwa kuwa ni Panya Road wa kundi la Taifa Jipya katika kituo cha Polisi cha Chang’ombe wilayani Temeke jana baada ya kukamatwa juzi wakileta vurugu na kupora watu kwa kutumia mapanga kwenye tamasha la kuibua vipaji lililofanyika Uwanja wa Zakhiem Mbagala.
 Vijana wanaotuhumiwa kuwa ni Panya Road wakiwa wameshika mapanga huku nyuma kukiwa na bango la kundi lao la Taifa Jipya walipofikishwa katika kituo cha Polisi cha Chang’ombe wilayani Temeke jijini Dar es Salaam jana.
 Vijana wanaotuhumiwa kuwa ni Panya Road wakiwa ndani ya gari la polisi tayari kwa kupelekwa rumande kwa ajili ya kusubiri siku ya kuepelekwa mahakamani kusikiliza kesi inayowakabili.
 Vijana wanaotuhumiwa kuwa ni Panya Road wakiwa ndani ya gari la polisi tayari kwa kupelekwa rumande kwa ajili ya kusubiri siku ya kuepelekwa mahakamani kusikiliza kesi inayowakabili.

Na ELISA SHUNDA,DAR
Kwa mujibu wa sheria ya watoto ya mwaka 2009 kifungu cha 7-9 wazazi na walezi wanawajibu wa kuwalea watoto wao katika mazingira mazuri ambayo hayatawasababishia madhara ya kiakili na kisaikolojia, udhalilishaji na kuhakikisha wanapata mahitaji ya elimu, afya na mavazi hivyo sheria inamtaka kila mzazi au mlezi kuhakikisha kuwa mtoto wake yupo salama muda wote dhidi ya udhalilishaji wa hatari zote ili watoto hao wakue vizuri.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Kanda ya Kipolisi ya Mkoa wa Temeke,Gilles Murato, alisema kuwa jeshi hilo limewakawata vijana 14 wa Panya Road ambao wanatuhumiwa kujihusisha na uvamizi kwenye Tamasha la kuinua vipaji lililoandaliwa na Clouds FM kwenye Viwanja vya Zakhiem eneo la Mbagala kwa kupora mali za wananchi na kuwashambulia baadhi ya raia kwa kutumia silaha aina ya mapanga.

Aidha kamanda Murato alisema kuwa kutokana na wazazi au walezi hao kukiuka sheria ya uangalizi wa malezi kwa watoto hao na iko wazi kuwa wazazi au walezi wanapaswa kuhakikisha watoto wao wako salama dhidi ya udhalilishaji wa aina yoyote ili vijana hao wakue vizuri kwa mujibu wa kifungu cha sheria cha 14, mzazi yeyote atakayeshindwa kutekeleza  hayo atafikishwa mahakamani na akitiwa hatiani atapewa adhabu ya kifungo cha miezi 6 jela au kulipa faini ya Sh.5,000,000.

"Tunawashukuru wananchi wa Buza kwa kutupa ushirikiano wa kuwakamata wahalifu hawa tunawaomba waendelee na ushirikiano huo kwa jeshi la polisi ili kuweza kukabiliana na vijana hao ambao wamekuwa wakifanya vitendo viovu dhidi ya raia", Alisema Murato.

Kwa upande wa wazazi waliofikishwa kutuoni hapo walisema wanasikitishwa na tabia za vijana wao kujingiza katika makundi yha kihalifu huku wakisema hawakua wakijua kama watoto wao ni Panya Road.

Ernest Chalo ambaye ni mmoja wa wazazi hao alisema anashangazwa  kwa kupewa taarifa ya mtoto wake kuwa amefariki
kwa kupigwa na wakazi hao  baada ya wananchi kumgundua kuwa mmoja wa kundi hilo la wahalifu Panya Road.

"Nime sikitishwa na kitendo cha mtoto wangu kujiingiza katika kundi hilo na kupewa taarifa amefariki dunia lakini alizinduka katika chumba cha maiti Mochwari hali ya kuwa alijua mtoto huyo alishauawa kwa uhalifu aliyoufanya".alisema Chalo.

Salumu Ally ambaye pia ni mmoja wa wazazi hao alisema mtoto wake ni mmoja wa kijana wanaoshikiliwa katika uhalifu wa kundi hilo  la panya Road hivyo kama mzazi anasikitishwa na tabia ya mtoto huyo kujiingiza katika kundi hilo hali ya kuwa nyumbani kuonekjana mtihifu.

" Kiukweli tabia ya kujihusisha na kuwa mshiriki wa kundi hili ni hali inayomsababishia mzazi kupatwa na ugonjwa wa moyo kutokana na mwenendo ambao mtoto anaoufanya bila wazazi kujua hayo,"alisema Ally.

Pia watuhumiwa hao walikiri mbele ya waandishi wa habari kujihusisha  na  makosa hayo kwa kujiingiza katika kundi
hilo la panya raod na kuonyesha baadhi ya silaha  walizokuwa wanatumia kufanyia matukio ya kihalifu.

Tukio la kuwepo kwa vijana wanaofahamika kwa jina la Panya Road siyo la kwanza kutokea wilayani humo hali inayosababisha baadhi ya wakazi wa Temekekuishi kwa hofu hivyo jeshi hilo limewataka wakazi wa maeneo hayo kushirikiana nao kwa kutoa taarifa ili kuondoa uhalifu huo katika wilaya yao hiyo iwe katika amani. 

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top