Slaus Technologies Tz1
 

Harakati za jiji Harakati za jiji Author
Title: ARIBU KUONA KAMA INAKUWAJE
Author: Harakati za jiji
Rating 5 of 5 Des:
Kumekuwa na taarifa iliyoenea kwenye mitandao ya kijamii kwamba Wakazi wa Jumbi, Wilaya ya kati Unguja wiki mbili baada ya mazishi ya m...

Kumekuwa na taarifa iliyoenea kwenye mitandao ya kijamii kwamba Wakazi wa Jumbi, Wilaya ya kati Unguja wiki mbili baada ya mazishi ya mtu mmoja kugundua kuwa mtu aliyezikwa yupo mtaani na anaonekana katika mazingira ya kutatanisha, na hivyo kuamua kwenda kulifukua kaburi na kukutana na majanga hayo hapo kama picha zinavyoonesha.

Tumefuatilia suala hili kwa undani zaidi inasemekana taarifa hizo hazina ukweli lakini taarifa iliyo sahihi ni kwamba,
   
taarifa ya kufukuliwa kaburi imetokea Bungi na siyo Jumbi kama ilivyodaiwa.

Hata hivyo hakuna mtu aliyekufa na kuzikwa kisha kuonekana mitaani kama taarifa zinavyosema.

Kilichotokea ni kwamba wametokea watu wasiojulikana wameenda porini kisha kuchimba shimo mfano wa kaburi na kuzika vitu vinavyosadikiwa kuwa vya ushirikina.

Shimo lilifukuliwa chini ya usimamizi wa polisi na maafisa wengine wa kiserikali na hakupatikana mtu aliyezikwa hapo.

Chanzo-http://www.zanzinews.com/

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top