Na Frank Wandiba
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul
Makonda amewataka wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam kutunza mazingira hasa sehemu
zenye mazalia ya mbu ili kuepukana na ugonjwa wa mabusha na matende.Makonda
ametoa wito huo siku ya leo.
Akizungumza na wananchi wa Kata
ya Buguruni wakati akizindua kampeni ya uhamasishaji unywaji dawa na
kufanyiwa upasuaji kwa magonjwa yasiyopewa kipaumbele ambayo ni Matende,
Mabusha, Kichocho, Minyoo na Usubi, ambapo kwa mujibu wa takwimu zinaonesha
wakazi wa Dar es Salaam wamekuwa wakisumbuliwa na magonjwa hayo hasa minyoo,
matende na mabusha.
Mhe Makonda alisema ni vyema
wakazi wa Dar es Salaam wakaitumia fursa hiyo ya kampeni itakayodumu kwa siku
tano kuanzia mpaka Oktoba 30, kwa kujitokeza kwa wingi kupimwa na kunywa dawa
kutaisaidia serikali kuinua nguvu kazi hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi kwani
watu wakiugua maradhi hayo bila ya kupata tiba au kuwa na kinga mapema hupoteza
nguvu kazi.
Mhe Makonda aliongeza kuwa
takribani ya watu 6400 wamegundulika na mabusha hivyo ni vyema wakawahi mapema
kupatiwa matibabu pamoja na kutoa wito kwa wenanchi wa mkoa wa dar na maeneo ya
jiarani wajitokeze kwa wingi hili kuweza kupita lengo la idadi ya wananchi
milioni 3.9 waliojitokeza wakati wa zoezi hilo mwaka 2009.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam Dokta Grace Maghembe amewataka wakazi hao kutosikiliza
upotoshaji wa kuwa wakitumia dawa hizo hawatakuwa na uwezo wa kupata watoto na
badala yake wajitokeze kwa wingi kwani dawa hizo ni salama, huku akisisitiza
kuwa kwa zoezi la unywaji wa dawa litafikia tamati Oktoba 30, wakati zoezi la
upasuaji litakuwa likiendelea mpaka
mwezi Desemba.
Bi Maghembe Alisema zoezi la upasuaji
kwa watu wenye mabusha linaloendelea kituo kilichopo Pugu zaidi ya watu 76 wameshapatiwa
matibabu aidha amelibainisha katika kuhalikisha
wanasogeza huduma hiyo karibu zaidi kwa wananchi wamejipanga kuongeza vituo
vingine kuendesha zoezi hilo katika maeneo mengine ya jiji la dar.
Post a Comment