Na Kijakazi Abdalla, Zanzibar
Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar imetumia kiasi ya dola 90 elfu kuifanyia matengenezo ya
kawaida Meli ya MV Mapinduzi ll iliyopelekwa Chelezoni Mombasa.
Akizungumza
na waandishi wa Habari Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na
Usafirishaji Mustafa Abuod Jumbe mara baada ya kuwasili Bandarini Malindi
amesema itaanza safari zake za kawaida Pemba kuanzia kesho ili kupunguza
usumbufu wa usafiri uliojitokeza baada ya kuondoaka meli hiyo.
Alisema
kuwa meli hiyo imefanyiwa matengenezo ya kawaida na hakuna kitu kilicho
badilishwa na baada ya matengenezo hayo itakuwa chini ya Mamlaka ya
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutoka kwa udhamini wa mtengenezaji.
Hata hivyo
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji amesema hivi
sasa Serikali imo katika mchakato wa kununua meli nyengine mbili mpya,
moja kwa ajili ya abiria na mizigo na nyengine itakuwa ya mafuta
Mapema
Nahodha wa Meli hiyo Abdulrahman Mzee amesema matengenezo ya meli
yaliyofanyika yamekwenda sambamba na muda uliopangwa na yamefanywa kwa
hali ya ubora kabisa
Amesema kuwa
kufanyika kwa matengenezo ya meli hiyo ni jambo la kawaida kwa chombo chochote
cha usafiri jambo linalokipa ubora chombo husika.
Meli ya MV
Mapinduzi ll iliondoka Zanzibar wiki mbili zilizopita kwenda chelezoni
Mombasa na imerejea Zanzibar leo kupitia Pemba ikiwa
imechukua abiria 1200 pamoja na mizigo
Post a Comment