Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam akitoa neon la utangulizi kwa Mgeni Rasmi Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa wakati wa sherehe za kilele cha Maadhimisho ya Miaka 55 tangu Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam kianzishwe, sherehe hizo zimefanyika katika ukumbi wa
Nkrumah, Kampasi ya Mwalimu J. K. Nyerere (Mlimani) mapema hii leo.
Naibu Katibu Mkuu
wa Wizara
ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard
Akwilapo akimkaribisha Mgeni Rasmi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
wakati wa sherehe za kilele cha Maadhimisho ya Miaka 55 tangu Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam kianzishwe, sherehe hizo zimefanyika katika ukumbi wa Nkrumah,
Kampasi ya Mwalimu J. K. Nyerere (Mlimani) mapema hii leo.
Mgeni Rasmi Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa akihutubia wanajumuiya ya Chuo
Kikuu Cha Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati wa sherehe za kilele cha
Maadhimisho ya Miaka 55 tangu Chuo hicho kianzishwe, sherehe hizo zimefanyika
katika ukumbi wa Nkrumah, Kampasi ya Mwalimu J. K. Nyerere (Mlimani) mapema hii
leo.
Baadhi ya wageni waalikwa
wakimsikiliza kwa makini Mgeni Rasmi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (hayupo
pichani) wakati akihutubia wanajumuiya
ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kwenye sherehe za kilele cha Maadhimisho
ya Miaka 55 tangu Chuo hicho kianzishwe, sherehe hizo zimefanyika katika ukumbi
wa Nkrumah, Kampasi ya Mwalimu J. K. Nyerere (Mlimani) mapema hii leo.
Mgeni Rasmi Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa akizindua kitabu kiitwacho “From Limumba Street to the Hill and
Beyond” wakati wa sherehe za kilele cha Maadhimisho ya Miaka 55 tangu Chuo
hicho kianzishwe, sherehe hizo zimefanyika katika ukumbi wa Nkrumah, Kampasi ya
Mwalimu J. K. Nyerere (Mlimani) mapema hii leo.
Na: Frank Shija, MAELEZO.
UDSM washauriwa kutumia
maadhimisho ya miaka 55 tangu kuanzishwa kwa Chuo hicho kufanya tathmini ya
mafanikio na changamoto walizokumbana nazo katika kipindi kilichopita ili
kujiwekea malengo ya maendeleo ifikapo 2061.
Rai hiyo imetolewa na Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (MB) katika hafla
ya kufunga maadhimisho ya miaka 55 ya
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) yaliyofanyika katika ukumbi wa Nkurumah leo
Jijini Dar es Salaam.
“Leo ni siku ambayo
tunahitimisha Maadhimisho ya miaka 55 tangu kuanzishwa kwa Chuo hiki, ni vyema
basi tukatumia sherehe hizi kufanya tathmini ya mafanikio na changamoto
mlizokumbana nazo kwa kipindi kilichopita”. Alisema Mhe. Majaliwa.
Awali akisoma hotuba yake
Waziri Mkuu Majaliwa alitumia fursa hiyo kuelezea namna ambavyo Serikali ya
Awamu ya Tano ilivyojipanga kuhakikisha inafanya maboresho makubwa katika
taasisi za elimu za umma ikiwamo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Alizitaja baadhi ya changamoto
na namna ambavyo Serikali imekuwa ikizishughulikia kuwa ni pamoja na; Maslahi
ya watumishi, wanataalamu na waendeshaji ambapo alisema Serikali inatambua
uwepo wa madai mbalimbali ikiwa ni pamoja na malimbikizo ya mishahara, na
kuongeza kuwa suala hilo tayari limekwisha anza kushughulikiwa kwa kuchukua
hatua kadhaa ikiwemo zoezi la uhakiki wa wafanyakazi na watumishi hewa.
Kuhusu changamoto ya uhaba wa
Wahadhiri Waandamizi na Maprofesa katika Vyuo vya Umma, Majaliwa alisema
Serikali itaendelea kuweka kipaumbele cha upatikanaji wa fedha za kutosha kwa
ajili ya mafunzo na kuvitaka Vyuo navyo viweke taratibu na mipango endelevu ya
kurithishana ili kupunguza ombwe lililopo.
Akizungumzia kuhusu mikopo ya
Elimu ya Juu, Waziri Mkuu amesema kuwa tayari Serikali kupitia Mhe. Rais Dkt.
John Pombe Magufuli imetoa ufafanuzi wa
namna utekelezaji wa kutoa mikopo hiyo, na Wizara yenye dhamana inaendelea na
uhakiki wa taarifa za waombaji wa mikopo. Alitoa wito kwa wanufaika na waombaji
wote wa mikopo wahakikishe wanawasilisha taarifa sahihi na za uhakika.
Nakuongeza kuwa Serikali
imekwisha ongeza bajeti ya mikopo ya Elimu ya Juu kutoka shilingi bilioni 340
mwaka 2015/2016 hadi bilioni 483 kwa mwaka 2016/2017 hivyo hakuna mwanafunzi
anyestahili kupata mkopo atakayekosa.
Awali akisoma historia ya chuo
hicho Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala
alisema kuwa maadhimisho hayo wanayatumia kufanya tathmini ya safari ya Chuo
kuelekea maendeleo ya karne moja ifikapo mwaka 1961.
Profesa Rwekaza amesema kuwa
kumekuwa na mabadiliko makubwa katika ukuaji wa Chuo hicho uliotokana na
mahitaji kulingana na wakati husika na kuongeza kuwa lengo kubwa la uongozi ni
kuhakikisha Chuo hicho kinaendela kuwa kinara katika kutoa elimu bora kulingana
na wakati.
Aliongeza kuwa pamoja na
changamoto kadhaa walizokumbana nazo Chuo hicho kimekuwa daraja muhimu la
kuzalisha wanataaluma ambapo takribani wanataaluma 90,000 wa ndani na nje ya
nchi wametokana na chuo hicho.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akizungumza kwa
niaba ya Waziri wa Wizara hiyo, Profesa Joyce Ndarichako amesema kuwa Serikali
itaendelea kushughulikia changamoto zinazoikabili sekta ya elimu nchini.
Ameongeza kuwa wizara imekuwa
ikiendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuhudumia sughuli mbalimbali za maendeleo
ya elimu na kuongeza kuwa hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
aliweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa mabweni ambao unatarajiwa
kukamilima ifikapo Desemba 2016.
Mradi huo utakapokamilika
utakuwa upunguza changamoto ya uhaba wa mabweni kwa wanafunzi na kuwaondolea
hadha ya kuishi mitaa, huku mabweni hayo yakitarajiwa kutumiwa na wanafunzi
takribani 3840.
Chuo kikuu cha Dar es Salaa
kinaadhimisha miaka 55 tangu kuasisiwa kwake mnamo mwaka 1961 huku kikianzia
katika majengo ya TANU( sasa hivi CCM) yaliyoko mtaa wa Lumumba jijini Dar es
Salaam kabla ya kuhamia katika eneo la Mlimani mnamo mwaka 1964.
Post a Comment