Slaus Technologies Tz1
 

Harakati za jiji Harakati za jiji Author
Title: SCORPION AFUTIWA MASHTAKA NA AFUNGULIWA MASHTAKA UPYA
Author: Harakati za jiji
Rating 5 of 5 Des:
Mahakama ya Wilaya ya Ilala, imemfungulia mashtaka mapya Salum Njwete (Scorpion).Amefunguliwa mashtaka mengine yanayofanana na ya awali...
Mahakama ya Wilaya ya Ilala, imemfungulia mashtaka mapya Salum Njwete (Scorpion).Amefunguliwa mashtaka mengine yanayofanana na ya awali ya unyang’anyanyi wa kutumia silaha.

Hata hivyo Njwete amekana shtaka na kurudishwa rumande,huku Hakimu Flora Haule anayesimamia kesi hiyo akizuia dhamana.

Awali Mahakama hiyo ilimfutia mashtaka yanayomkabili Scorpion baada ya upande wa mashtaka kuomba shtaka hilo liondolewe mahakamani kwa sababu hawana nia ya kuendelea na kesi hiyo na kutokana na maombi hayo, Hakimu Adelf Sachore alikubaliana na ombi hilo kwa kuzingatia kifungu namba 91 kifungu kidogo cha kwanza cha sheria ambacho kinampa Mamlaka Mkurugenzi Wa Mashtaka nchini (DPP) kuondoa shtaka mahakamani muda wowote ili mradi kama kesi hiyo haijatolewa hukumu.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top